Jinsi ya kutengeneza mabanda bora kwaajili ya kufugia kuku
Jinsi ya kutengeneza mabanda bora kwaajili ya kufugia kuku.
Habari ndugu msomaji leo ningeanza kutoa elimu ya namna ya kutengeneza mabanda bora kwaajili ya kufugia kuku.Karibu sana.
Mabanda ya kuku yaliyo bora ni muhimu sana katika kuku walio bora na wenye afya. Mabanda mabovu pia huweza kusababisha hasara katika mradi hasa katika vipindi vya baridi na joto kali. Mabanda ya kuku yaliyo bora hutakiwa angalau kufikisha miaka 10 toka yalipo tengenezwa.Tuanze kama ifuatavyo:
.Vitu muhimu vya kuzingatia katika kutengeneza mabanda ya kuku
-Chagua eneo la wazi ambalo lipo mbali na shamba lingine(uzalishaji mwingine), mbali na makutano ya barabara, na mijini. Pia kuwe na geti la kuingia na kutoka kirahisi katika mabanda ya kuku.
- Sambaza umeme na maji katika banda la kuku. Zungushia banda kwa uzio wa waya ili kuzuia wanyama wengine kuingia ndani ya banda la kuku.
- Kama utahitaji kuweka miti kwaajili ya kivuli hakikisha hautumii miti ya matunda kama vile miembe, mipera n.k
-Pia sakafia banda la kuku ili kurahisisha wakati wa kusafisha.Ila hakikisha kabla ya kuweka kuku katika banda hili ambalo limesakafiwa weka vitu ambavyo vitazuia ubaridi kutoka kwenye sakafu kwenda kwa kuku. Tumia maranda ya mbao,pumba za mchele, pumba za mahindi n.k
-Umbali unaohitajika kutoka banda moja kwenda lingine na kutoka kwenye mti wa kivuli na banda ni mita 25.
-Tengeneza banda kuelekeza upande mashariki-magharibi ili kuingiza mwanga wa jua katika kiasi kinachohitajika katika banda.
Vipimo maalum kwa ajili ya banda la kuku.
- Kuku 10 aina ya broilers(kuku wa nyama) wanaweza kuwekwa katika mita ya mraba 1 (1m²).
- Kuku 6-8 aina ya layers(kuku wa mayai) wanaweza kuwekwa katika mita ya mraba 1(1m²) wenye umri wa wiki 18-20.
- Kuku 5-6 aina ya layers(kuku wa mayai) kwenye mita ya mraba 1(1m²) ambao wamekomaa(mature layers).
Vipimo
Eneo 50m²
Broilers 500
Layers 250
Upana ni 5m
Urefu ni 10m
Eneo 100m²
Broilers 1000
Layers 500
Upana 6m
Urefu 17m
Eneo 200m²
Broilers 2000
Layers 1000
Upana 7m
Urefu 30m
Vyombo muhimu katika banda la kuku.
Vyombo kwaajili ya chakula(Feeders)
Kuna aina nyingi ya feeders kutokana na umri na aina ya kuku.Tumia aina ya feeders kulingana na umri na aina ya kuku ulionao.
Vyombo kwaajili ya maji(Drinkers)
Pia hapa zipo aina nyingi za drinkers kulingana na umri wa kuku.Zipo ndogo kwaajili ya vifaranga na kubwa kwaajili ya kuku wakubwa. Tumia drinkers nzuri zisizovuja ili kuzuia unyevu katika banda la kuku ambao ni hatari hasa kwa vifaranga.
Vyombo kwaajili ya joto(Heating equipments)
Unaweza kutumia jiko la mkaa, umeme n.k kuweka joto katika banda la kuku.Joto ni muhimu katika ukuaji wa kuku hvyo ni muhimu kuweka vyanzo vya joto katika banda. Hakikisha pia joto lisizidi wala kupungua liwe wastani.Kiasi cha joto kinachohitajika ni kulingana na eneo ambalo umetengeneza banda,kuna maeneo yenye baridi kali na mengine yenye joto hivyo weka joto katika banda kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.
Hapo juu nimeeleza namna ya kutengeneza mabanda ya kuku, ndugu msomaji usikose makala ijayo kujua namna ya kutotolesha vifaranga na kuwakuza katika asilimia kubwa. Karibu.
Usiache kufatilia blog hii kwa elimu mbalimbali za ufugaji wa aina zote.
Kwa msaada zaidi waweza nipigia kwa namba 0713945958.
Ahsante.
Comments
Post a Comment