Jinsi ya kutengeneza mabanda bora kwaajili ya kufugia kuku
Jinsi ya kutengeneza mabanda bora kwaajili ya kufugia kuku. Habari ndugu msomaji leo ningeanza kutoa elimu ya namna ya kutengeneza mabanda bora kwaajili ya kufugia kuku.Karibu sana. Mabanda ya kuku yaliyo bora ni muhimu sana katika kuku walio bora na wenye afya. Mabanda mabovu pia huweza kusababisha hasara katika mradi hasa katika vipindi vya baridi na joto kali. Mabanda ya kuku yaliyo bora hutakiwa angalau kufikisha miaka 10 toka yalipo tengenezwa.Tuanze kama ifuatavyo: .Vitu muhimu vya kuzingatia katika kutengeneza mabanda ya kuku - Chagua eneo la wazi ambalo lipo mbali na shamba lingine(uzalishaji mwingine), mbali na makutano ya barabara, na mijini . Pia kuwe na geti la kuingia na kutoka kirahisi katika mabanda ya kuku. - Sambaza umeme na maji katika banda la kuku. Zungushia banda kwa uzio wa waya ili kuzuia wanyama wengine kuingia ndani ya banda la kuku. - Kama utahitaji kuweka miti kwaajili ya kivuli hakikisha hautumii miti ya matunda kam...